Posts

Showing posts from March, 2024

35 Twende kwake

​ 1.    Twende kwake, twende kwake, kwake Yesu sasa, Sasa twende kwake, kwake Yesu sasa!   2.    Akwokoe, akwokoe, Bwana Yesu sasa! Sasa akwokoe, Bwana Yesu, sasa!   3.    Msadiki, msadiki, Bwana Yesu sasa, Sasa msadiki, Bwana Yesu sasa!   4.    Anaweza, anaweza, Bwana Yesu sasa, Sasa anaweza, Bwana Yesu sasa!   5.    Anapenda, anapenda, Bwana Yesu sasa, Sasa anapenda, Bwana Yesu sasa!   6.    Njoo hima, njoo hima, kwake Yesu sasa, Sasa njoo hima, kwake Yesu sasa!

36 Anisikiaye aliye yote

​ 1.    Anisikiaye, aliye yote; Sasa litangae, wajue wote, Duniani kote neno wapate, Atakaye na aje! Chorus: Ni “Atakaye,” ni “atakaye,” Pwani hata bara, na litangae; Ni Baba Mpenzi alinganaye Atakaye na aje.   2.    Anijiliaye, Yesu asema, Asikawe, aje hima mapema; Ndimi njia, Kweli, ndimi Uzima;   3.    Atakaye aje, ndiyo ahadi; Atakaye hiyo, haitarudi! Atakaye lake, ni la abadi! Atakaye na aje.

37 Waitwa, mwovu, na Bwana

​ 1.   W aitwa, mwovu, na Bwana Umwendee hima sana, Usafiwe dhambi zako, Humwoni ni mwema kwako? Chorus: Unaitwa! Itika tu! Umwendee Bwana Yesu! Sifiche makosa yako, Uungame dhambi zako! Kristo tu umuamini, Ndiyo njia ua Mbinguni.   2.    Alilipa damu yake Alikufa yeye Bwana, Mimi nawe tuwe wema.   3.    Ukifanywa kuwa mwema Utaingia rahani Na wapenzi wa zamani.   4.    Ni mwanga tu, nchi ile, Kwamba wataka ufike Sharti huku uosheke.

38 Twende kwa Yesu

​ 1.    Twende kwa Yesu mimi nawe, Njia atwonya tuijue Imo Chuoni; na Mwenyewe, Hapa asema, Njoo!   Chorus: Na furaha tutaiona, Mioyo ikitakata sana, Kwako, Mwokozi, kuonana, Na milele kukaa.   2.    “Wana na waje”, atwambia, Furahini mkisikia, Ndiye mfalme wetu pia, Na tumtii, Njoo.   3.    Wangojeani? Leo yupo; Sikiza sana asemapo; Huruma zake zikiwapo, Ewe kijana, Njoo.

39 Mwenye dhambi huna raha

​ 1.    Mwenye dhambi huna raha, Sikiza nakusihi, Utapata msamaha Kwake Yesu Mwokozi! Njoo hima, njoo hima, Naye atafurahi.   2.    Yesu anakwita sana Naye yuko Mbinguni; Hofu ya kifo hapana Kwake ukiamini. Njoo hima, njoo hima, Utapata amani.   3.    Hatakwita siku zote; Ni ya sasa nafasi. Lete na uchafu wote, Kukawa haipasi. Njoo hima, njoo hima, Ni wokovu halisi.   4.    Uzima uko kwa Bwana Twae uzima hasa Bure unapatikana, Wokovu twae sasa! Njoo hima, njoo hima, Twae utakatifu.