125 Ati twonane Mtoni?

1. Ati twonane mtoni?

Maji mazuri ya Mbingu;
Yanatokea mwangani,
Penye kiti cha Mungu.

Naam, twonane mtoni!
Watakatifu, kwenu ni mtoni!
Tutakutanika mtoni
Penye kiti cha Mungu. 
 
2. Tukitembea mtoni
Na Yesu mchunga wetu
Daima tu ibadani
Usoni pake kwetu.
 
3. Kwang’ara sana mtoni
Cha Mwokozi ni kioo,
Milele hatuachani,
Tumsifu kwa nyimbo.
 
4. Si mbali sana mtoni,
Karibu tutawasili,
Mara huwa furahani
Na amani ya kweli.

Comments

Popular posts from this blog

37 Waitwa, mwovu, na Bwana

52 Yote namtolea Yesu

41 Yesu aliniita