126 Ni mji mzuri

1. Ni mji mzuri,

Mbali sana;
Watu wanawiri
Kama jua;
Waimba kwa tamu,
Tuna wema hakimu:
Sifa na idumu,
Kwake Bwana. 
 
2. Ni mji mzuri
Twende sote!
Una na fahari
Msikawe!
Raha tutaona,
Dhambi hapana tena;
Hatutaachana
Siku zote.
 
3. Ni mji mzuri;
Macho yote
Huko wanawiri
Kama pete;
Baba tutamwona,
Tukifanywa tu wana;
Tumo kupendana
Naye sote. 
 
4. Ni mji mzuri;
Tusipotee
Na tuwe hodari,
Tuupate!
Tufunze, tutume
Kwa taji na ufalme:
Sifa na zivume
Siku zote.

Comments

Popular posts from this blog

37 Waitwa, mwovu, na Bwana

52 Yote namtolea Yesu

41 Yesu aliniita