129 Karibu na wewe

1. Karibu na wewe,

Mungu wangu
Karibu zaidi,
Bwana wangu
Siku zote niwe
Karibu na wewe,
Karibu zaidi
Mungu wangu.
 
2. Mimi nasafiri
Duniani,
Pa kupumzika
Sipaoni,
Nilalapo niwe
Karibu na wewe,
Karibu zaidi
Mungu wangu.
 
3. Na kwa nguvu zangu
Nikusifu;
Mwamba, uwe maji
Ya wokovu;
Mashakani niwe
Karibu na wewe;
Karibu zaidi
Mungu wangu.
 
4. Na nyumbani mwa juu,
Baba yangu,
Zikikoma hapa
Siku zangu,
Kwa furaha niwe
Pamoja na wewe,
Karibu kabisa
Mungu wangu.

Comments

Popular posts from this blog

37 Waitwa, mwovu, na Bwana

52 Yote namtolea Yesu

41 Yesu aliniita