139 Nuru ya rohoni

1. Nuru ya rohoni

ni Bwana Yesu.
Nakuomba sana
niangazishe;
ukanitazame
kwa huruma tu,
 
ukanitulize
mimi maskini.
 
2. Futa dhambi zangu
kwa damu yako.
Hasira ya Mungu
iniondoke.
Machubuko yako,
hata mateso,
 
niyawaze vema
rohoni mwangu.
 
3. Nakutumaini
peke yako tu,
niwe mtumwa wako
pote nilipo
utanikubali
sina mashaka!
 
Nitakushukuru
pasipo mwisho.

Comments

Popular posts from this blog

37 Waitwa, mwovu, na Bwana

52 Yote namtolea Yesu

41 Yesu aliniita