141 Pana jito, lina maji mazuri

1. Pana jito, lina maji Mazuri,

Yaenda ulimwenguni.
Lametameta nalo Linang’aa.
Walijua jito hilo?
 
Ninakuita nawe njoo!
Utafute jito hilo!
Maji yake yapoza Moyo.
Nawe yateke unywe.
 
2. wanywao maji haya wafurahi,
waimba kwa shangwe kubwa.
Makosa na shida Yanaondoshwa,
Wote waoshwa na Bwana.
Ninakuita nawe njoo …
 
3. Jito hilo latoa maji mengi,
matamu yapendezayo.
Yaponya wagonjwa, Yatia nguvu,
Uchafu watakashika.
Ninakuita nawe njoo …
 
4. maji ya jito hilo ni uzima
unaotoka Kwa Yesu.
Damu yake yenye kiasi kikuu
Imemwagwa tusafike.
Ninakuita nawe njoo …

Comments

Popular posts from this blog

37 Waitwa, mwovu, na Bwana

52 Yote namtolea Yesu

41 Yesu aliniita