144 Mbele ninaendelea

1. Mbele ninaendelea,

ninazidi kutembea.
Maombi uyasikie,
Ee Bwana, unipandishe.
 
Ee, Bwana, uniinue,
Kwa imani nisimame;
Nipande milima yote,
Ee Bwana,
Unipandishe.
 
2. Sina tamani nikae,
Mahali pa shaka, kamwe;
Hapo wengi wanakaa,
Kuendelea naomba.
 
3. Nisikae duniani,
asumbuapo Shetani;
Natazamia mbinguni,
nitafika na amani.
 
4. Nataka nipandishwe juu,
Zaidi yale mawingu.
Nitaomba nifikishwe,
Ee Bwana unipandishe.

Comments

Popular posts from this blog

37 Waitwa, mwovu, na Bwana

52 Yote namtolea Yesu

41 Yesu aliniita