103 Kaa nami

1. Kaa nami, ni usiku tena;

Usiniache gizani, Bwana;
Msaada wako haukomi;
Nili peke yangu, kaa nami. 
 
2. Siku zetu hazikawi kwisha,
Sioni la kunifurahisha;
Hakuna ambacho hakikomi,
Usiye na mwisho kaa nami.
 
3. Nina haja nawe kila saa;
Sina mwingine wa kunifaa;
Mimi nitaongozwa na nani
Ila wewe? Bwana, kaa nami.
 
4. Sichi neno uwapo karibu;
Nipatalo lote, si taabu;
Kifo na kaburi haviumi;
Nitashinda kwako, kaa nami.
 
5. Nilalapo nikuone wewe,
Gizani mote nimulikiwe;
Nuru za mbinguni hazikomi,
Siku zangu zote kaa nami. 

Comments

Popular posts from this blog

37 Waitwa, mwovu, na Bwana

52 Yote namtolea Yesu

41 Yesu aliniita