106 Mungu awe nanyi daima

1. Mungu awe nanyi daima,

Hata twonane ya pili,
Awachunge kwa fadhili,
Mungu awe nanyi daima. 
 
Hata twonane huko juu,
Hata twonane kwake kwema;
Hata twonane huko juu,
Mungu awe nanyi daima. 
 
2. Mungu awe nanyi daima;
Ziwafunike mbawaze,
Awalishe, awakuze;
Mungu awe nanyi daima.
 
3. Mungu awe nanyi daima;
Kila wakati wa shani
Awalinde hifadhini;
Mungu awe nanyi daima.
 
4. Mungu awe nanyi daima;
Awabarikie sana,
Awapasulie kina;
Mungu awe nanyi daima.

Comments

Popular posts from this blog

37 Waitwa, mwovu, na Bwana

52 Yote namtolea Yesu

41 Yesu aliniita