107 Ewe Baba wa Mbinguni

1. Ewe, Baba wa Mbinguni,

Usikie twombalo
Hapa chini duniani,
Na uwe radhi nalo
 
Ee Mungu, bariki
Ndugu hawa wawili!
Ee Mungu, bariki
Ndugu hawa wawili!
 
2. Watu hawa mbele zako,
Na mbele ya kanisa;
Watimize Neno lako
Wanakutana sasa.
 
3. Kama Yesu na Kanisa,
Ni mmoja, na hivyo,
Watu hawawape sasa
Wawe mmoja vivyo
 
4. Walinde, Bwana, daima,
Wabariki nyumbani
Uwape nyingi salama
Humu ulimwenguni.
 
5. Wabariki, ewe Bwana,
Watu hawa wawili,
Wape upaji wa wana,
Wafurahishwe kweli.
 
6. Siku za duniani
Zitakapopungua,
Wape kurithi Mbinguni
Mema ya kwendelea.


Comments

Popular posts from this blog

37 Waitwa, mwovu, na Bwana

52 Yote namtolea Yesu

41 Yesu aliniita