109 Nitaimba ya Yesu

1. Nitaimba ya Yesu,

Kwa rehema zake,
Baraka nyingi sana
Nimepata kwake;
Nitaimba ya Yesu,
Sadaka ya Mungu,
Alimwaga damu
Ukombozi wangu.
 
2. Nitaimba ya Yesu
Hapa siku zote,
Nitakapokumbuka
Vyema vyake vyote;
Nitaimba ya Yesu
Hata mashakani,
Yeye atanilinda
Mwake ubavuni.
 
3. Nitaimba ya Yesu
Niwapo Njiani;
Takaza Mwendo, hata
Nifike Mbinguni;
Nikiisha ingia
Mlangoni mle,
Yesu nitamwimbia
Mbinguni milele.

Comments

Popular posts from this blog

37 Waitwa, mwovu, na Bwana

52 Yote namtolea Yesu

41 Yesu aliniita