49 Nitwae hivi nilivyo

1.  Nitwae hivi nilivyo,

Umemwaga damu yako,
Nawe ulivyoniita,
Bwana Yesu, naja, naja.
 
2.  Hivi nilivyo; si langu
Kujiosha roho yangu;
Nisamehe dhambi zangu,
Bwana Yesu, naja, naja.
 
3.  Hivi nilivyo; sioni
Kamwe furaha moyoni;
Daima ni mashakani,
Bwana Yesu, naja, naja.
 
4.  Hivi nilivyo kipofu,
Maskini na mpungufu;
Wewe u mtimilifu;
Bwana Yesu, naja, naja.
 
5.  Nawe hivi utanitwaa;
Nisithubutu kukawa,
Na wewe hutanikataa,
Bwana Yesu, naja, naja.
 
6.  Hivi nilivyo; mapenzi
Yamenipa njia wazi;
Hali na mali sisazi,
Bwana Yesu, naja, naja.

Comments

Popular posts from this blog

37 Waitwa, mwovu, na Bwana

52 Yote namtolea Yesu

41 Yesu aliniita