Posts

Showing posts from February, 2024

40 Nasikia kuitwa

​ 1.    Nasikia kuitwa Na sauti yako Nikasafiwe kwa damu Ya kwangikwa kwako. Chorus: Nimesogea Mtini pako, Unisafi kwa damu ya kwangikwa kwako.   2.    Ni mnyonge kweli, Umenipa nguvu, Ulivyonisafi taka, Ni utimilivu.   3.    Yesu hunijuvya; Mapenzi imani, Tumai, amani, radhi, Hapa na Mbinguni.   4.    Huipa imara, Kazi yake, ndani: Huongezeka neema, Ashindwe Shetani.   5.    Huishuhudia, Mioyo ya imani Ya kuzipata ahadi, Wakimuamini.   6.    Napata wokovu, Wema na neema; Kwako Bwana nina nguvu Na haki daima.

41 Yesu aliniita

​ 1.    Yesu aliniita, “njoo, Raha iko kwangu, Kichwa chako ukilaze Kifuani mwangu.” Nilikwenda kwake mara, Sana nilichoka, Nikapata kwake raha, Na furaha tena.   2.    Yesu aliniita, “njoo, Kwangu kuna maji, Maji ya uzima, bure, Unywe uwe hai, ” Nilikwenda kwake mara Na maji nikanywa; Naishi kwake, na kiu Kamwe sina tena.   3.    Yesu aliniita, “njoo, Dunia ni giza, Ukinitazama nuru Takung’arizia.” Nilikwenda kwake mara Yeye jua langu, Ni kila wakati mwanga Safarini mwangu.

42 Kivulini mwa Yesu

​ 1.    Kivulini mwa Yesu kuna Kituo: Kituo mbali na hamu, kituo kilicho tamu.   Chorus: Kivulini mwa Yesu kuna kituo; Kivulini mwa Yesu kuna kituo; Raha tu, mle; amani tupu. Furaha tele; kivulini mwa Yesu Raha tu, mle; amani tupu, Furaha tele; kivulini mwa Yesu.   2.    Kivulini mwa Yesu nina amani Iliyopita fahamu, tena itakayodumu.   3.    Kivulini mwa Yesu nina furaha; Furaha yenye fahari, ya kueneza habari.

43 Yesu akwita

​ 1.    Yesu akwita, chanena Chuo; Uje leo, uje leo; Kwani kusita? Akwita, Njoo; Unatanga upeo. Chorus: Hwita leo, hwita leo. Yesu akwita kwa pole akwita leo.   2.    Waliochoka, wapumzike, Hwita leo, hwita leo: Wenye mizigo, wakamtweke, Wapate mapumuo.   3.    Anakungoja, uliye yote, Uje leo, uje leo; Uliyekosa usijifiche: Woshwe, uvikwe nguo.   4.    Yesu asihi wakawiao, Waje leo, waje leo. Watafurahi waaminio; Usije kwani? Njoo.

44 Kukawa na giza dunia yote

​ 1.    Kukawa na giza dunia yote, Ni Mwanga wa ulimwengu, Ikaisha ulipokuja yote, Ni mwanga wa ulimwengu.   Chorus: Jua, Yesu hana mwenziwe! Nalipofuka kama wewe; Nakwombea umwone nawe, Ni mwanga wa ulimwengu.   2.    Hatuna giza tudumuo mwake, Ni mwanga wa ulimwengu; Tumwandamiapo nyayoni mwake Ni mwanga wa ulimwengu.   3.    Enyi wa gizani wenye kutanga! Ni Mwanga wa ulimwengu, Kaulekeeni, mpate lenga; Ni mwanga wa ulimwengu.   4.    Tutamwona Mwokozi juu ya mbingu Ni Mwanga wa ulimwengu; Ni nuru za mbingu Kondoo wa Mungu Ni mwanga wa ulimwengu.

45 Mtazame Huyo! Aliyeangikwa juu

​ 1.    Mtazame Huyo! Aliyeangikwa juu Hivi sasa upate ishi. Mwenye – dhambi dhaifu, mtazame tu Wala usifanye tashwishi. Chorus: Tazama! Tazama! Tazama uishi! Mtazame huyo aliyeangikwa juu Hivi sasa upate ishi.   2.    Kama Mwana Kondoo hakuondoa dhambi, Na makosa yako maovu! Kama deni zetu zote hakulipa Mbona imemwagika damu?   3.    Si kutubu na sala ikomboayo, Ila damu ndiyo salama; Na aliyeimwaga aweza, sasa, Dhambi zako kukufutia.   4.    Usiwe na shaka, Mungu amesema, Hakuna alilolisaza; Hapo alipokuja alitimiza Kazi zote alizoanza.   5.    Basi twae uzima kwa kufurahi Upokee kwa Bwana, sasa; Ujijue hakika kwake kuishi Yesu aishiye kabisa.

46 Twae wangu uzima

​ 1.    Twae wangu uzima, Sadaka ya daima; Twae saa na siku Zikutukuze huku.   2.    Twae mikono nayo, Ifanye upendavyo, Twae yangu miguu Kwa wongozi wako tu.   3.    Twae sauti yangu, Niimbe kwa Mungu tu; Itwae na midomo, Ijae neno lako.   4.    Twae dhambi pia, Na yote ya dunia; Twae yangu hekima, Upendavyo tumia.   5.    Njia itwae, Mungu, Haitakuwa yangu; Twae moyo; ni wako, Uwe makazi yako.   6.    Twae mapenzi yangu, Sifa za moyo wangu; Twae kabisa nafsi Nniwe wako halisi.

47 Ni wako wewe

​ 1.    Ni wako wewe, nimekujua, Na umeniambia; Lakini Bwana, nataka kwako,  Nizidi kusongea. Chorus: Bwana vuta, vuta, nije nisongee, Sana, kwako mtini. Bwana vuta, vuta nije, nisongee, Pa damu ya thamani.   2.    Niweke sasa nikatumike Kwa nguvu za neema;\ Uyapendayo nami nipende, Nizidi kukwandama.   3.    Nina furaha tele kila saa Nizungumzayo kwako, Nikuombapo nami napata  Kujua nia yako.   4.    Mapenzi yako hayapimiki, Ila ng’ambo ya liko. Anasa pia sitazijua, Bila kufika kwako.

48 Naweka dhambi zangu

​ 1.    Naweka dhambi zangu Juu yake Bwana Kuziondoa, kwangu Hulemea sana; Na uaili wangu Ameuondoa; Dawa yangu ni damu, Kwa hiyo napoa.   2.    Na uhitaji wangu Nitamjuvisha, Kwa upungufu wangu Yeye anatosha; Majonzi yangu yote Na mizigo yangu, Atachukua vyote Yesu Bwana wangu.   3.    Na roho yangu nayo, Imechoka sana; Namletea hiyo Ilindwe na Bwana; Ni jema jina lake, Nalo lapendeza, Imanweli na kwake Tutalitukuza.   4.    Natamani daima Niwe kama Bwana, Mpole, tena mwema, Wa mapenzi sana; Zaidi natamani Kwenda kwake juu, Nikaone mbinguni Enzi yake kuu.

49 Nitwae hivi nilivyo

​ 1.    Nitwae hivi nilivyo, Umemwaga damu yako, Nawe ulivyoniita, Bwana Yesu, naja, naja.   2.    Hivi nilivyo; si langu Kujiosha roho yangu; Nisamehe dhambi zangu, Bwana Yesu, naja, naja.   3.    Hivi nilivyo; sioni Kamwe furaha moyoni; Daima ni mashakani, Bwana Yesu, naja, naja.   4.    Hivi nilivyo kipofu, Maskini na mpungufu; Wewe u mtimilifu; Bwana Yesu, naja, naja.   5.    Nawe hivi utanitwaa; Nisithubutu kukawa, Na wewe hutanikataa, Bwana Yesu, naja, naja.   6.    Hivi nilivyo; mapenzi Yamenipa njia wazi; Hali na mali sisazi, Bwana Yesu, naja, naja.

50 Yesu nakupenda, U mali yangu

​ 1.    Yesu nakupenda, U mali yangu, Anasa za dhambi sitaki kwangu; Na Mwokozi aliyeniokoa, Sasa nakupenda, kuzidi pia.   2.    Moyo umejaa mapenzi tele Kwa vile ulivyonipenda mbele, Uhai wako ukanitolea Sasa nakupenda, kuzidi pia.   3.    Ulipoangikwa Msalabani Tusamehewe tulio dhambini; Taji ya miiba uliyoivaa, Sasa nakupenda, kuzidi pia.   4.    Niwapo hai, niwapo maiti, Kupendana nawe kamwe siachi; Hari za kifo zikinienea, Sasa nakupenda, kuzidi pia.   5.    Mawanda mazuri, na maskani Niyatazamapo huko Mbinguni, Tasema na taji nitakayovaa Sasa nakupenda, kuzidi pia.

51 Mungu twatoa shukrani

​Mungu twatoa shukrani, Kwa kutulinda usikuni, Na kutuangalia mchana, Kutuongoza kila mara.

52 Yote namtolea Yesu

​ 1.    Yote namtolea Yesu Nampa moyo wote, Nitampenda siku zote, Namwandama kila saa. Chorus: Yote kwa Yesu, Yote kwa Yesu, Yote kwako, Ee mwokozi, Natoa sasa.   2.    Yote namtolea Yesu, Nainamia pake; Nimeacha na anasa, Kwako Yesu nipokee,   3.    Yote namtolea Yesu, Nifanye niwe wako; Nipe Roho yako, Bwana, Anilinde daima. 4.    Yote namtolea Yesu, Nami naona sasa; Furaha ya ukombozi, Nasifu jina lake.

53 Wewe umechoka sana

​ 1.    Wewe umechoka sana? Wataka raha? Kwake Yesu utapata furaha.   2.    Alama anazo Yeye? Sasa! makovu  Ya mikono, na miguu, Na mbavu.   3.    Nacho kimevikwa taji Kichwa cha huba? Alivikwa taji kweli miiba.   4.    Huku nikimtafuta nipate nini? Maonjo nje na ndani amani.   5.    Kwamba namwandama Bwana, Mwisho ni nini? Ni furaha na salama Mbinguni.

54 Yesu nataka kutakaswa sana

​ 1.    Yesu nataka kutakaswa sana, Nataka moyo uwe enzi yako. Ukiangushe kilichoinuka Unioshe sasa niwe mweupe. Chorus:   Mweupe tu, ndiyo mweupe, Ukiniosha nitakuwa safi.   2.    Bwaba Yesu, unitazame sasa, Unifanye niwe dhabihu hai; Najitoa kwako, na moyo wote; Unioshe sasa niwe mweupe.   3.    Bwana kwa hiyo nakuomba sana, Nakungojea miguuni pako, Naomba unioshe damuni tu, Unioshe sasa niwe mweupe.   4.    Bwana ninadumu kukungojea, Niumbie moyo safi, Ee Mungu, Wanaokujia hutupi kamwe, Unioshe sasa niwe mweupe.

55 Nipe moyo wenye sifa

​ 1.    Nipe moyo wenye sifa Sio wa utumwa; Moyo ulionyunyizwa Damu ya thamani.   2.    Moyo maskini, moyo Wa kunyenyekea, Moyo utawaliwao Na Mwokozi pia.   3.    Mwenye kutubu, mnyonge, Sadiki, amini; Kamwe, kamwe asitengwe Akaaye ndani.   4.    Mpya, mwema na mawazo Mwingi wa mapenzi Nawe uwe kielelezo Moyo wa Mwokozi.   5.    Ni uule moyo wako; Moyo wa huruma Yesu, natamani kwako Kukujua vyema.   6.    Na ya midomo matunda Yako, nipe nami; Amani isiyokoma Iwe yangu mimi.   7.    Nitie yako tabia, Inishukie juu; Jina lako nipe pia, Ndilo la pendo tu.   8.    Ni wa Baba utukufu; Mwana atukuke; Na roho Mtakatifu U Utatu pweke.

56 Ni siku kuu siku ile

​ 1.    Ni siku kuu siku ile Ya kumkiri Mwokozi! Moyo umejaa tele, Kunyamaza hauwezi. Chorus: Siku kuu! Siku kuu! Ya kuoshwa dambi zangu kuu! Hukesha na kuomba tu, Ananiongoza miguu. Siku kuu! siku kuu! Ya kuoshwa dhambi zangu kuu.   2.    Tumekwisha kupatana Mimi wake, Yeye wangu, Na sasa nitamwandama, Nikiri neno la Mungu.   3.    Moyo tulia kwa Bwana Kiini cha raha yako, Huna njia mbili tena; Yesu ndiye njia yako.   4.    Nadhiri yangu ya mbele Nitaiweka daima, Hata ije siku ile, Ya kwonana kwa salama.

57 Naendea Msalaba

​ 1.    Naendea Msalaba, Ni mnyonge na mpofu, Yapitayo naacha, Nipone Msalabani. Chorus:   Nakutumaini tu, Ewe Mwana wa Mungu; Nainamia kwako; Niponye, Mponya wangu.   2.    Nakulilia sana: Nalemewa na dhambi; Pole Yesu asema; “Nitazifuta zote”.   3.    Natoa vyote kwako, Nafasi nazo nguvu, Roho yangu na mwili, Viwe vyako milele.   4.    Kwa damu yake sasa, Nimegeuka roho, Nikaziacha tamaa Nimfuate Yesu tu.   5.    Yesu yuaja tena! Nimepevuka kwake, Kila chembe kamili; Msifuni yeye mponya!

58 Mwamba wenye imara

​ 1.    Mwamba wenye imara Kwako nitajificha! Maji hayo na damu Yaliyotoka humu, Hunisafi na dhambi, Hunifanya mshindi.   2.    Kwa kazi zote pia , Sitimizi sharia. Nijapofanya bidii, Nikilia na kudhii, Hayaishi makosa; Ndiwe wa kuokoa.   3.    Sina cha mkononi, Naja Msalabani; Nili tupu, nivike; Ni mnyonge, nishike; Nili mchafu naja, Nioshe nisijafa.   4.    Nikungojapo chini, Nakwenda kaburini; Nipaapo Mbinguni, Na kukwona enzini: Roho yangu na iwe Rahani mwako wewe.

59 Peleleza ndani yangu

​ 1.    Peleleza ndani yangu, Iwe safi nia, Kwangu kama kwako  Mungu, Idhihiri pia.   2.    Peleleza moyo wangu Unifunulie, Yaliyomo ndani yangu Nami niyajue.   3.    Kwanza washe zako tambi, Kumefunga giza; Nijue ambavyo dhambi Ni la kuchukiza.   4.    Peleleza na mawazo Ni mbegu za mambo, Asili ya machukizo, Maumbuo – umbo.   5.    Zidi kuyapeleleza Katikati yangu Hata wishe nifundisha Udhaifu wangu.   6.    Hapo nikikwinamia Mbele zako, Mungu, Hakika nitakujua U Mpenzi wangu.

60 Waponyeni watu wamo kifoni

​ 1.    Waponyeni watu wamo kifoni, Watoeni walio shimoni; Na aangukaye mumzuie; Ya Bwana Yesu wahubirini. Chorus:   Walio kifoni waokoeni, Mwokozi yuko, wahubirini.   2.    Wajapokawia anangojea, Awasubiri waje tobani; Msiwadharau, muwaonyeni; Huwasamehe; wakiamini.   3.    Myoyoni mwa ndani, yule shetani Ameyaseta mawazo yao; Lakini kwa Bwana huwa mazima, Tukiwavuta kwa pole hao.   4.    Kawaokoeni, waje njiani, Mutimize mapenzi ya Bwana; Na kwa nguvu zake warudi kwake, Kwa subira waonyeni sana.