Posts

Showing posts from August, 2023

99 Maelfu na maelfu

​ 1. Maelfu na maelfu Wenye nguo bora! Masafu ya waongofu Wenye na bendera! Amekwisha kamili Vita vya shetani Fungueni lango hili; Njoni, ingieni!    2. Imbeni aleluya, Zipae Mbinguni! Pigeni sana sauti Kwa kutumaini! Kwa hiyo viliumbwa Nchi hata Mbingu Dhiki za muda zikisha, Asifiwe Yesu.   3. Loo! Tukionana Pwani ya ng’amboni! Loo! Tukishirikiana Milele Mbinguni! Midomo yote pia, Huko itaimba Wajane kufufukiwa Na kila yatima!   4. Himiza enzi yako, Uliyetufia Utimize watu wako, Wakosaji pia, Mpendwa wa taifa twakutumaini! Uzifunue ishara Urudi enzini! 

100 Tumrudie Bwana

​ 1. Mbona washangaa njiani? Mbona warejea nyuma? Warudi tena gizani Alimokutoa Bwana?    2. Ni ya bure yote haya, Uliyofunzwa ya Mungu? Ni bure amekufia Bwana Yesu kwa uchungu?   3. Wamtia kristo aibu Na maneno yake pia? Siku yaja ya hesabu, Utamjibuje Bwana?   4. Upandapo tena hayo, Halafu utayavuna. Rudi kwa Bwana upesi, Mwombe akupokee tena. 

101 Twonane milele

​ 1. Nyimbo na tuziimbe tena Za alivyotupenda mbele; Kwa damu ya thamani sana! Mbinguni twonane milele.    Twonane milele, Twonane bandarini kule; Twonane milele, Twonane bandarini kule.    2. Hupozwa kila aoshwaye, Kwa damu ya Kondoo yule; Ataishi afurahiye Vya Yesu mbinguni milele.   3. Hata sasa hufurahia Tamu yake mapenzi yale, Je, kwake tukifikilia, Kutofarakana milele?   4. Twende mbele kwa jina lake, Hata aje mwokozi yule, Atatukaribisha kwake, Tutawale naye milele.   5. Sauti zetu tuinue Kumsifu Mwokozi yule, Ili watu wote wajue Wokovu u kwake milele. 

102 Kazi yangu ikiisha

​ 1. Kazi yangu ikiisha, nami nikiokoka; Na kuvaa kutokuharibika, Nitamjua Mwokozi nifikapo ng’amboni; Atakuwa wa kwanza kunilaki.   Nitamjua, nitamjua, nikimwona uso kwa uso; Nitamjua, nitamjua, kwa alama za misumari.    2. Furaha nitapata nikiona makao Bwana aliyotuandalia; Nitamsifu mwokozi kwa rehema na pendo Vilivyonipa pahali Mbinguni.   3. Nao waliokufa katika Bwana Yesu, Nitawaona tena huko juu; Lakini nifikapo kwake huko Mbinguni, Nataka kumwona Mwokozi kwanza.   4. Milangoni mwa mji Bwana atanipitisha, Pasipo machozi wala huzuni. Nitauimba wimbo wa milele; lakini Nataka kumwona Mwokozi kwanza. 

103 Kaa nami

​ 1. Kaa nami, ni usiku tena; Usiniache gizani, Bwana; Msaada wako haukomi; Nili peke yangu, kaa nami.    2. Siku zetu hazikawi kwisha, Sioni la kunifurahisha; Hakuna ambacho hakikomi, Usiye na mwisho kaa nami.   3. Nina haja nawe kila saa; Sina mwingine wa kunifaa; Mimi nitaongozwa na nani Ila wewe? Bwana, kaa nami.   4. Sichi neno uwapo karibu; Nipatalo lote, si taabu; Kifo na kaburi haviumi; Nitashinda kwako, kaa nami.   5. Nilalapo nikuone wewe, Gizani mote nimulikiwe; Nuru za mbinguni hazikomi, Siku zangu zote kaa nami. 

104 Twasoma ni njema sana

​ 1. Twasoma, ni njema sana Mbinguni, kwa Bwana; Twasoma, dhambi hapana, Mbinguni kwa Bwana; Malaika wema wako, Vinanda vizuri viko, Na majumba tele yako, Mbinguni kwa Bwana.    2. Siku zote ni mchana, Ni nchi ya raha; Wala machozi hapana, Ni nchi ya raha; Walioko wanuona Uso wa Mwokozi, tena Jua jingine hapana, Ni nchi ya raha.   3. Nyama na vitu viovu Havimo kabisa; Kifo nacho, na ubovu, Havimo kabisa. Ni watakatifu wote, Wameoshwa dhambi zote; Wasiosafiwa wote Hawamo kabisa.   4. Tuna dhambi, pia sote, Mwokozi akafa; Kwake tutaoshwa zote, Mwokozi akafa; Kwake twapata wokovu, Tutawona utukufu; Mbinguni tutamsifu; Mwokozi akafa.   5. Baba, mama, ndugu zetu, Twendeni kwa Bwana; Huku chini sio kwetu, Twendeni kwa Bwana; Tusishikwe na dunia, Na dhambi kutulemea; Tutupe vya chini pia, Twendeni kwa Bwana. 

105 Kuwatafuta

​ 1. Kuwatafuta wasioweza, Kuomba wamrejee Yesu, Kuwaambia maneno yake, “Njooni kwangu, nawapenda”.    Nitakwenda, (kwenda), niwatafute Waongofu (wa Bwana) wageuke, Waingie (wote) katika zizi La Mkombozi (wetu) Yesu kristo.    2. Kuwatafuta wasioweza, Waonyeshwe Mwokozi wetu, Kuwaongoza, wapate wote Uzima wa milele.   3. Kazi hiyo nataka kufanya, Leo nimesikia mwito Kuwainua waangukao, Waletwe kwake Yesu njia.

106 Mungu awe nanyi daima

​ 1. Mungu awe nanyi daima, Hata twonane ya pili, Awachunge kwa fadhili, Mungu awe nanyi daima.    Hata twonane huko juu, Hata twonane kwake kwema; Hata twonane huko juu, Mungu awe nanyi daima.    2. Mungu awe nanyi daima; Ziwafunike mbawaze, Awalishe, awakuze; Mungu awe nanyi daima.   3. Mungu awe nanyi daima; Kila wakati wa shani Awalinde hifadhini; Mungu awe nanyi daima.   4. Mungu awe nanyi daima; Awabarikie sana, Awapasulie kina; Mungu awe nanyi daima.

107 Ewe Baba wa Mbinguni

​ 1. Ewe, Baba wa Mbinguni, Usikie twombalo Hapa chini duniani, Na uwe radhi nalo   Ee Mungu, bariki Ndugu hawa wawili! Ee Mungu, bariki Ndugu hawa wawili!   2. Watu hawa mbele zako, Na mbele ya kanisa; Watimize Neno lako Wanakutana sasa.   3. Kama Yesu na Kanisa, Ni mmoja, na hivyo, Watu hawawape sasa Wawe mmoja vivyo   4. Walinde, Bwana, daima, Wabariki nyumbani Uwape nyingi salama Humu ulimwenguni.   5. Wabariki, ewe Bwana, Watu hawa wawili, Wape upaji wa wana, Wafurahishwe kweli.   6. Siku za duniani Zitakapopungua, Wape kurithi Mbinguni Mema ya kwendelea.

108 Twenenda sayuni

​ 1. Mpendao Bwana Ije raha yenu! Imbeni nyimbo za raha Wa ibada yenu.    Twenenda Sayuni, Mji mzuri Sayuni; Twenenda juu Sayuni Ni maskani ya Mungu.    2. Wasiimbe wao wasioamini, Watoto wa Mungu ndio waimbao chini.   3. Twaona rohoni Baraka za Mungu, Tusijafika Mbinguni Kwenye utukufu.   4. Tutakapo mwona Masumbuko basi, Huwa maji ya uzima, Anasa halisi.   5. Tupaaze sauti, Na fute machozi, Twenenda kwa Imanweli Naye ni Mwokozi.

109 Nitaimba ya Yesu

​ 1. Nitaimba ya Yesu, Kwa rehema zake, Baraka nyingi sana Nimepata kwake; Nitaimba ya Yesu, Sadaka ya Mungu, Alimwaga damu Ukombozi wangu.   2. Nitaimba ya Yesu Hapa siku zote, Nitakapokumbuka Vyema vyake vyote; Nitaimba ya Yesu Hata mashakani, Yeye atanilinda Mwake ubavuni.   3. Nitaimba ya Yesu Niwapo Njiani; Takaza Mwendo, hata Nifike Mbinguni; Nikiisha ingia Mlangoni mle, Yesu nitamwimbia Mbinguni milele.

110 Mapya ni mapenzi hayo

​ 1. Mapya ni mapenzi hayo, Asubuhi tunayo, Saa za giza hulindwa Kwa uzima kuamshwa.   2. Kila siku, Mapya pia Rehema, wema, na afya, Wokofu, na msamaha, Mawazo mema, furaha.   3. Tukijitahidi leo Na mwendo utupasao, Mungu atatueleza Yatakayompendeza.   4. Mambo yetu ya dunia Mungu atayang’aria, Matata atageuza Yawe kwetu ya Baraka.   5. Yaliyo madogo, haya Mungu tukimfanyia, Yatosha: tutafaidi Huvuta kwake zaidi.   6. Ewe Bwana, siku zote, Tusaidie kwa yote: Mwendo wetu wote vivyo, Uwe kama tuombavyo.

111 Neno lako Bwana

​ 1. Neno lako, Bwana, Ni imara sana; Lilo latwongoza, Lilo latufunza.   2. Adui wabaya Wakikaribia, Neno lake Bwana Ni ulinzi sana.   3. Siku za dhoruba Soma ukiomba; Neno lake Bwana Msaada sana.   4. Ukiliamini, Hwenda na amani; Una na furaha Neno ni siraha.   5. Ni furaha kweli, Na wingi wa mali, Neno lake Bwana Kwa wasiokana   6. Neno la rehema, Tukali wazima; Faraja I papo, Tufarikanapo.   7. Tulijue sana Neno lako, Bwana, Hapa tukupende, Kisha kwako twende.

112 Nilikupa wewe maisha yangu

​ 1. Nilikupa wewe Damu ya moyoni, Ili wokolewe, Winuke ufuni: Nimekunyimani? Umenipa nini?   2. Nilikupa miaka Yangu duniani Upate inuka, Kuishi Mbinguni: Nimekunyimani? Umenipa nini:   3. Niliacha nuru Za Baba, Mbinguni, Kwingia taabu Za ulimwenguni: Nimekunyimani? Umenipa nini?   4. Niliteswa sana, Mateso kifoni, Usije yaona Hayo ya motoni: Nimekunyimani? Umenipa nini?   5. Nimekuletea Huku duniani Upendo na afya Zatoka Mbinguni: Nimekunyimani? Umenipa nini?   6. Nipe siku zako, Udumu mwangani; Na taabu yako, Wingie rahani Nafsi, pendo, mali, Twae Imanweli.

113 Ni mfalme wa mapenzi

​ 1. Ni Mfalme wa mapenzi Ndiye anichungaye, Sipungukiwi, hawezi. Kunipoteza yeye.   2. Kando ya mji mazima Yeye huniongoza Katika malisho mema Daima hunilaza.   3. Mara nyingi hupotea Kwa ukaidi wangu, Naye huniandamia, Hunirudisha kwangu.   4. Uvulini mwa mauti, Siachi hatari kamwe, Wewe Bwana huniachi, Mwokozi wangu wewe.   5. Waniandikia meza Neema kwako tele. Kwa wewe, yote naweza. Na msalaba mbele.   6. Kamwe hautapungua Uule wema wako; Mwisho, atanichukua, Juu, niimbe kwako.

114 Bwana Mungu, nashangaa kabisa

​ 1. Bwana Mungu, nashangaa kabisa Nikitazama kama vilivyo Nyota, ngurumo, vitu vingi vyote viumbwavyo kwa uwezo wako. Roho yangu na ikuimbie Jinsi Wewe ulivyo Mkuu, Roho yangu na ikuimbie Jinsi Wewe ulivyo Mkuu.    2. Nikitembea pote duniani, Ndege huimba, nawasikia, Milima hupendeza macho sana, Upepo nao nafurahia.    3. Nikikumbuka kama Wewe Mungu Ulivyompeleka Mwanao, Afe azichukue dhambi zetu, Kuyatambua ni vigumu mno.    4. Yesu Mwokozi utakaporudi Kunichukua kwenda Mbinguni, Nitashukuru na kwimba milele, Wote wajue jinsi ulivyo. 

115 Kilima kando ya Mji

​ 1. Kilima kando ya mji Alikufa Bwana; Kuokoa wakosaji Akateswa sana.   2. Kabisa hayasemeki, Mateso dhaifu Alikufa mwenye Haki Tupate wokovu.   3. Alimwaga damu yake Ili tuwe wema, Tufae kukaa kwake Mbinguni daima.   4. Hatuna mwenye imani Aliye na haki, Wa kutosha yetu deni, Rafiki Yesu tu.   5. Alijua peke yake Kufungu Mbingu Ufunguo damu yake Kondoo wa Mungu.   6. Aliyetupenda hivyo Nasi tumpende, Tukamtumai vivyo Na kazi tutende.

116 Bwana , U sehemu yangu

​ 1. Bwana u sehemu yangu, Rafiki yangu wewe; Katika safari yangu Tatembea na wewe; Pamoja na wewe, Pamoja na wewe, Katika safari yangu Tatembea na wewe.    2. Mali hapa sikutaka, Ili niheshimiwe, Na yanikute mashaka Sawa sawa na wewe, Pamoja na wewe, Pamoja na wewe, Heri nikute mashaka Sawasawa na wewe.   3. Niongoze safarini, Mbele unichukue Mlangoni kwa Mbinguni Niingie na wewe. Pamoja na wewe, Pamoja na wewe, Mlangoni kwa mbinguni, Niingie na wewe.

117 Tufani inapovuma

​ 1. Tufani inapovuma Sana moyoni mwangu, Huona pa kujificha Mkononi mwa Mungu.    Hunificha, hunificha Adui hatanipata, Hunificha, hunificha, Mkononi mwake.    2. Pengine kuna taabu Yanisongeza kwake; Naijua si hasira, Ni ya mapenzi yake.   3. Adui wakiniudhi Nami nikisumbuka, Mungu atavigeuza Vyote viwe baraka.   4. Niishipo duniani Ni tufani daima, Anilindapo rohoni Nitakaa salama.

118 Ni ujumbe wa Bwana

​ 1. Ni ujumbe wa Bwana, Aleluya! wa maisha ya daima, Amenena mwenyewe, Aleluya! Utaishi ukitazama.   Tazama, ishi sasa! Kumtazama Yesu, Amenena mwenyewe, Aleluya! Utaishi ukitazama.   2. Ni ujumbe wa wema, Aleluya! Nawe shika, rafiki yangu! Ni habari ya raha Aleluya! Mwenye kuinena ni Mungu.   3. Uzima wa daima,Aleluya ! Kwake Yesu utauona. ukimtazama tu, Aleluya! Wokovu u pweke kwa Bwana.

119 Si damu ya nyama

​ 1. Si damu ya nyama Iliyomwagika Iwezayo kuondoa Dhambi za wakosa.    2. Yeye Bwana Yesu Sadaka ya Mungu, Mwenye damu ya thamani, Ni mwokozi kweli.   3. Kwa imani yangu, Namshika yeye, Naziweka dhambi zangu Juu ya kichwa chake.   4. Mzigo wa dhambi Sichukui tena, Ameuchukua yeye, Juu ya msalaba.   5. Bwana Yesu ndiye, Mwokozi wa kweli Tumsifu siku zote, Twapata uhuru.