Posts

Showing posts from July, 2023

120 Enyi wanadamu

1. Enyi wanadamu mbona Sana mwatanga-tanga, Kama kondoo wanyonge, Wasio na mchunga? Yuko mchunga mmoja Mwenye mapenzi mema; Haya kutaneni kwake, Atawachunga vyema.    2. Mungu tunamwona kuwa Mwenye uwezo wote; Na nguvu zake zapita Mawazo yetu yote: Ni Baba,mapenzi yake Ni makubwa hakika; Hatuwezi kuyajua, Na hayana mpaka.   3. Rehema za Mungu nazo Zina upana sana; Kama huo wa bahari, Mwisho wake hapana; Haki yake ina mema, Kwa hayo twashukuru, Kwetu uko msamaha, Furaha na uhuru.   4. Mapenzi yake mapana, Sisi hatuna cheo Cha kutosha, nao moyo Una wema upeo; Ukombozi mwingi mno Katika damu yake; Sote twapata furaha, Kwa maumivu yake.    5. Yesu mkaribieni Njoni msife myoyo; Njoni kwake kwa imani, Mema yake ni hayo; Heri tuwe kama wana Tushike neno lake, Daima atujaza Tele furaha yake.

121 Liko lango moja wazi

​ 1. Liko lango moja wazi, Ni lango la mbinguni; Na wote waingiao Watapata nafasi.    Lango ndiye Yesu Bwana Wote waingie kwake, Lango! Lango La Mbinguni ni wazi.   2. Yesu ndiye lango hili, Hata sasa ni wazi, Kwa wakubwa na wadogo, Tajiri na maskini.   3. Hili ni lango la raha, Ni lango la rehema; Kila mtu apitaye Hana majonzi tena.   4. Tukipita lango hili Tutatua mizigo, Tuliochukua kwanza, Tutavikwa uzima.   5. Hima ndugu tuingie Lango halijafungwa, Likifungwa mara moja Halitafunguliwa.

122 Bwana Yesu

​ 1. Bwana Yesu, Bwana Yesu, Mbona unaumia? Unateseka sana, Kwa ajili ya kuomba, Waomba na jasho jingi likageuka damu.    Kumbe! Ni dhambi zangu zinazokuumiza. Bwana wangu, Mungu wangu, Mimi leo, naja kwako Ili niziungame.    2. Bwana Yesu, Bwana Yesu, Mbona unaumia, na mizigo mizito? Umejitwalia wewe, msalaba mabegani Kwa ajili ya watu.   3. Bwana Yesu, Bwana Yesu, Mbona unatukanwa, wawambwa kama mwizi, Bila kosa ukalia, Baba yangu, wasamehe, Chukua roho yangu.   4. Bwana Yesu, Bwana Yesu, Muda ulipofika, nchi ikawa giza, Mbinguni pakatulia, Angani pakawa kimya, Watu wakaogopa.   5. Bwana Yesu, Bwana Yesu, Jinsi ulivyoumwa, ukamwomba Baba, Leo umeshinda kifo, sasa wapaa Mbinguni, Naimba, Haleluya.

123 Nimeketi mimi nili kipofu

​ 1. Nimeketi mimi nili kipofu Gizani nangojea macho; Ewe Bwana Yesu mwenye wokovu, Ondoa dhambi zangu nzito. Huruma hakuna aonaye, Gizani nagojea macho, Sasa nitakase nikusihiye, Yesu, na dhambi zangu nzito.    2. Tangu siku nyingi nimepofuka Natamani uso nikwone; Ewe Bwana Yesu, mwenye baraka Sema neno, basi, nipone.   3. Nimeketi mimi nili na giza, Nami ya kutumai sina; Ili nasikia kunong’oneza, “Kwake Yesu kuna kupona.”

124 Mungu ulisema

​ 1. Mungu ulisema, Giza ilikoma; Twakushukuru! Twakusihi sote, Duniani mote Na kwa watu wote, Iwe nuru.    2. Yesu ulikuja, Ulituletea Nuru kuu; Macho kwa vipofu, Maisha kwa wafu; Twakushukuru.   3. Roho kiongozi, Roho wa mapenzi Tia nuru; Mwovu hata sasa Watu huwatosa, Tunakwomba hasa, Iwe nuru.   4. Mungu wa utatu Mwanga wao watu, Tuwe huru; Twende kote-kote Wafundishwe wote, Duniani mote, Iwe nuru.

125 Ati twonane Mtoni?

​ 1. Ati twonane mtoni? Maji mazuri ya Mbingu; Yanatokea mwangani, Penye kiti cha Mungu. Naam, twonane mtoni! Watakatifu, kwenu ni mtoni! Tutakutanika mtoni Penye kiti cha Mungu.    2. Tukitembea mtoni Na Yesu mchunga wetu Daima tu ibadani Usoni pake kwetu.   3. Kwang’ara sana mtoni Cha Mwokozi ni kioo, Milele hatuachani, Tumsifu kwa nyimbo.   4. Si mbali sana mtoni, Karibu tutawasili, Mara huwa furahani Na amani ya kweli.

126 Ni mji mzuri

​ 1. Ni mji mzuri, Mbali sana; Watu wanawiri Kama jua; Waimba kwa tamu, Tuna wema hakimu: Sifa na idumu, Kwake Bwana.    2. Ni mji mzuri Twende sote! Una na fahari Msikawe! Raha tutaona, Dhambi hapana tena; Hatutaachana Siku zote.   3. Ni mji mzuri; Macho yote Huko wanawiri Kama pete; Baba tutamwona, Tukifanywa tu wana; Tumo kupendana Naye sote.    4. Ni mji mzuri; Tusipotee Na tuwe hodari, Tuupate! Tufunze, tutume Kwa taji na ufalme: Sifa na zivume Siku zote.

127 Bwana Yesu atakuja

​ 1. Bwana Yesu atakuja, Vumilia! Omba, ukiwa na haja, Vumilia! Mbingunu Mungu aliko, Mwamini Mwokozi wako, Nawe utafika huko, Vumilia!    2. Ikikucheka dunia, Vumilia! Mwovu atakuvizia, Vumilia! Hataweza kukushinda, Bwana Yesu akulinda, Roho yako, akupenda, Vumilia!   3. Na ukiwa hatarini, Vumilia! Dhiki nyingi duniani, Vumilia! Vyatupasa kuyakuta, Majaribu na matata, Na Bwana hakutuficha; Vumilia!   4. Adui wakikutana, Vumilia! Na ndugu wakikukana, Vumilia! Zote, zote zitakwisha, Nguvu zote za kutisha Mungu chini atashusha; Vumilia!    5. Moyoni una majonzi, Vumilia! Ndiyo bonde-ya-machozi, Vumilia! Hima tutaandamana, Kwetu Mbinguni na Bwana Tena hatutaachana; Vumilia!

128 Mmoja apita wote

​ 1. Mmoja apita wote, Atupenda; Zaidi ya ndugu wote, Atupenda; Rafiki wa duniani, Wote hatuwaamini; Yesu kwa kila zamani, Atupenda.    2. Kumjua ni uzima, Atupenda; Jinsi ajaavyo wema Atupenda; Yeye ametununua Kwa damu aliyomwaga, Dhambini kutuokoa, Atupenda.   3. Sasa tunaye rafiki, Atupenda; Hupenda kutubariki; Atupenda; Twapenda kumsikia, Atwita kukaribia, Nasi tutamwamania, Atupenda.   4. Husamehe Dhambi zetu, Atupenda; Hushinda adui zetu, Atupenda; Anatwonea huruma, Hatupati ila mema, Anatwongoza salama, Atupenda. 

129 Karibu na wewe

​ 1. Karibu na wewe, Mungu wangu Karibu zaidi, Bwana wangu Siku zote niwe Karibu na wewe, Karibu zaidi Mungu wangu.   2. Mimi nasafiri Duniani, Pa kupumzika Sipaoni, Nilalapo niwe Karibu na wewe, Karibu zaidi Mungu wangu.   3. Na kwa nguvu zangu Nikusifu; Mwamba, uwe maji Ya wokovu; Mashakani niwe Karibu na wewe; Karibu zaidi Mungu wangu.   4. Na nyumbani mwa juu, Baba yangu, Zikikoma hapa Siku zangu, Kwa furaha niwe Pamoja na wewe, Karibu kabisa Mungu wangu.

130 Niongoze, Bwana Mungu

​ 1. Niongoze, Bwana Mungu, Ni msafiri chini; Ni mnyonge, nguvu sina: Nishike mkononi; U mkate wa Mbinguni, nilishe siku zote.    2. Kijito cha maji mema, Kitokacho mwambani, Nguzo yako, moto, wingu, Yaongoza jangwani; Niokoe mwenye nguvu; Nguvu zangu na ngao.   3. Nikikaribia kufa, Sichi neno lolote, Wewe kifo umeshinda Zinawe nguvu zote, Tutaimba sifa zako, Kwako juu milele.

131 Piga sana vita vyema

​ 1. Piga sana vita vyema Kwa ushujaa daima, Yesu ndiye nguvu zako, Yesu ndiye kweli yako.   2. Kaza mwendo, ushindane Angaza macho, umwone Yesu ndiye njia yako, Naye ndiye tuzo lako.   3. Tupa kizito, simama, Tazama mbele, si nyuma; Ni yeye uzima wako, Naye ni kipendo chako.   4. Tangamka, uamini Akushika mikononi Hageuki, akupenda, Kuwa naye una pia.

132 Sauti sikilizeni

​ 1. Sauti sikilizeni Za waimbao juu, “Aleluya, Aleluya, Aleluya, mkuu!” Wako makundi-makundi Kama nyota wang’ara, Kwa makuti ya mitende, Na meupe wamevaa.    2. Wazazi na manabii Wafanyaji wa njia; Mashahidi, waandishi, Nao wafalme pia! Mabikira kina-mama, Wajane wa kusali, Waimba wakikutana “Msifunu Imanweli”.   3. Watu toka huzunini Wameosha na nguo, Ni kwa damu yake Yesu; Maonjo, mbali nao! Walitekwa, walikatwa Hata kwa misumeno, Kwao kifo na shetani Walishindiwa mno.   4. Mungu mumo mwake Mungu, Nuru mumu mwa nuru, Kwa kufungamana mwako Tutaishi mahuru; Tujalize, Imanweli, Kujaa kwako wewe Mungu Baba, Mungu Mwana, Mungu Roho, tunawe.

133 Ni wako Mungu

​ 1. Ni wako Mungu! Ni furaha kwangu, Ni raha kumjua mwokozi wangu.    Aleluya enzi ndako; Aleluya,Amin. Aleluya,enzi ndako; Rejea Yesu.    2. Mwana wa Mungu Ndiye fungu langu, Na moyo hufurahi kwa Yesu wangu.   3. Raha ya kweli Ina jina hili, Na aliyeshika,ana Mbingu kweli.   4. Nimeingia Mapendano haya, Nimepata uzima na Mbingu pia.   5. Nilipo chini, Ni mwako kazini Hata nije kwako uliko Mbinguni.

134 Juu yake langu shaka

​ 1. Juu yake langu shaka, Yesu namuwekea, Nami sitafedheheka Nikimtegemea.    Natumai, natumai, Nnatumai kwake tu; Natumai, natumai, Natumai kwake tu.    2. Juu yake, dhambi zangu; Aniosha kwa damu; Nionekane kwa Mungu, Nisiye na laumu.   3. Juu yake yangu hofu; Kwake nimetulia; Sipotei kwa upofu Njia aning’azia.   4. Juu yake raha yangu; Humuangalia tu; Mwenye kila ulimwengu, Aniruzuku na huu.   5. Juu yake, moyo wangu; Hali yangu na mali; Mimi wake, Yeye wangu, Twapasana kamili.

135 Mapenzi ya milele

​ 1. Mapenzi ya milele Ndiyo yanipendezayo; Yalinipenda mbele, Sina fahamu nayo; Sasa amani yake Tele rohoni mwangu, Ni mimi kwa kuwa wake, Na yeye kuwa wangu, Ni mimi kuwa wake, Na yeye kuwa wangu   2. Mbingu zinang’ara juu, Na nchi nayo vivyo; Macho ya dunia tu Hayajaona hivyo; Nyuni huimba sana, Maua yana rangi, Ni kumjua Bwana Na pendo zake nyingi, Ni kumjua Bwana Na pendo zake nyingi,   3. Mambo mengi maovu Nayo yenye kutisha, Sasa hayana nguvu, Si yenye kututisha; Ni mkononi mwake, Nalindwa salamani Ninajua ni wake, Ni wake mapenzini. Ninajua ni wake, Ni wake mapenzini.   4. Wake hata milele, Si kutengana tena; Hunipa raha tele Moyoni mwangu, Bwana; Hiyo nchi na Mbingu Zitatoweka zile, Ni wake, Yeye wangu, Milele na milele. Ni wake, Yeye wangu, Milele na milele.

136 Msifuni, Yesu ndiye mkombozi

​ 1. Msifuni ,Yesu ndiye mkombozi; Imbeni ya pendo zake kuu, Sujuduni,malaika mlioko, Jina lake liwe na sifa kuu. Kama vile mchunga uchungavyo Vivyo sisi kutwa atachunga. Msifuni mlio wake watoto Msifuni aliye mchunga.    2. Msifuni,Yesu ndiye mkombozi; Akateswa tupate ongoka; Ndiye Mwamba,Dhamana ya kuokoka; Sujuduni kwake muangikwa, Yesu aliyeudhiwa na hamu Kwa pendo za baba yake Mungu. Aliyefyolewa na kusulubiwa. Msifuni ndilo letu fungu.   3. Msifuni,Yesu ndiye Mkombozi; Shindukeni,enyi malango juu; Bwana Yesu tangu milele Mwokozi, Mvikeni taji, ni yake tu. Atakuja kuitawala nchi, Yesu,Mwombezi wetu wa Mungu. Msifuni, ni mfalme wa salama; Ndiye kweli mwana wake Mungu.

137 Yesu mponya

​ 1. Yesu ndiye mganga wetu Aponya wagonjwa wote; Mganga wetu ni Yesu, Aponyaye hasira.    Tumsifu huyo Yesu Tumsifu milele, Kwani Mponya mtakata Mwokozi wa wanyonge   2. Mganga wetu ni Yesu Huondoa matusi; Mganga wetu ni Yesu, Mwenye kuponya choyo.   3. Mganga wetu ni Yesu Huponya wivu wetu; Yesu ndiye aponyae Kelele za nyumbani.   4. Mganga wetu ni Yesu Mponya wa tamaa mbaya; Mganga wetu ni Yesu Uasherati hufuta   5. Mganga wetu ni Yesu Aponya kiu cha pombe, Mganga wetu ni Yesu Kila dhambi uponya

138 Tukutendereza Yesu (Luganda)

​ 1. Yesu, Mulokozi wange: Lero nze wuwo wenka; Omusaigwo gunazi’za Yesu Mwana gwendiga.   Tukutendereza, Yesu, Yesu Mwana gwendiga; Omusaigwo gunazi’za; Nkwebaza, Mulokozi.   2. Eda nafuba bufubi Okufuna, emirembe; Lero maliride dala Okweyabiza Yesu.   3. Nababuliranga bantu Obulokozi bwona, Obutali bwa kitundu Obulamba obwobuwa   4. Nategezanga ebya Yesu Nobuvumunesitya; Eyanziya mu busibe Nokuwonya eyamponya.   5. Nebaza eyanunula nze; Eyamponya wa kisa! Yesu ankuma Ansanyusaera, Bulijo yebazibwe.

139 Nuru ya rohoni

​ 1. Nuru ya rohoni ni Bwana Yesu. Nakuomba sana niangazishe; ukanitazame kwa huruma tu,   ukanitulize mimi maskini.   2. Futa dhambi zangu kwa damu yako. Hasira ya Mungu iniondoke. Machubuko yako, hata mateso,   niyawaze vema rohoni mwangu.   3. Nakutumaini peke yako tu, niwe mtumwa wako pote nilipo utanikubali sina mashaka!   Nitakushukuru pasipo mwisho.

140 Mahali ni pazuri

​ 1. Mahali ni pazuri, ndugu wanapokaa, wakipatana vema, na wakipendana.   2. Kama umande mzuri, unyweshavyo shamba, vivyo na Mungu wetu, hubariki ndugu.   3. Upendano hujenga, boma zuri kwao, wakae na amani, waliookakoka.    4. Na ulimwengu wote, watiwa nuruni, halafu kundi moja, na mchunga mmoja tu. 

141 Pana jito, lina maji mazuri

​ 1. Pana jito, lina maji Mazuri, Yaenda ulimwenguni. Lametameta nalo Linang’aa. Walijua jito hilo?   Ninakuita nawe njoo! Utafute jito hilo! Maji yake yapoza Moyo. Nawe yateke unywe.   2. wanywao maji haya wafurahi, waimba kwa shangwe kubwa. Makosa na shida Yanaondoshwa, Wote waoshwa na Bwana. Ninakuita nawe njoo …   3. Jito hilo latoa maji mengi, matamu yapendezayo. Yaponya wagonjwa, Yatia nguvu, Uchafu watakashika. Ninakuita nawe njoo …   4. maji ya jito hilo ni uzima unaotoka Kwa Yesu. Damu yake yenye kiasi kikuu Imemwagwa tusafike. Ninakuita nawe njoo …

142 Babangu kule mbiguni.

​ 1. Babangu kule mbinguni, aliye juu pa malaika, aangalia njia zangu na kunilinda maisha.   2. Hata unywele kichwani hauanguki ovyo tu na siri zote za moyoni zajulikana kwa Baba.   3. Zamani nisipojua, amekwisha kuandika mkononi mwake jina langu, ndio upedo wake mkuu.   4. Ee Baba yangu u mwema, nami nataka kufanya kama malaika wafanyavyo mbinguni kwako milele!.

143 Nchi nzuri yametameta

​ 1. Nchi nzuri yametameta, Huonekana kule mbali, Naye Yesu hutuongoza. Tukafike na sisi huko.   Sisi mbali, karibu, Tutaimba na sisi huko!   2. Kule tutawaona wengi Wapendwao na Yesu Bwana, Tutashirikiana nao Itakuwa furaha kubwa. Si mbali..   3. Tutamwona na Bwana Wetu, Yesu kristo mwokozi Wetu, Tutashangilia daima, Tuna hamu ya kwenda Kwetu. Si mbali..

144 Mbele ninaendelea

​ 1. Mbele ninaendelea, ninazidi kutembea. Maombi uyasikie, Ee Bwana, unipandishe.   Ee, Bwana, uniinue, Kwa imani nisimame; Nipande milima yote, Ee Bwana, Unipandishe.   2. Sina tamani nikae, Mahali pa shaka, kamwe; Hapo wengi wanakaa, Kuendelea naomba.   3. Nisikae duniani, asumbuapo Shetani; Natazamia mbinguni, nitafika na amani.   4. Nataka nipandishwe juu, Zaidi yale mawingu. Nitaomba nifikishwe, Ee Bwana unipandishe.